Mkuu wa jeshi la Nigeria Luteni Jenerali Kenneth Minimah amesema
kuwa vita dhidi ya wanamgambo wa Boko Haram vitamalizika hivi karibuni.
Mkuu wa jeshi la Nigeria ameyasema hayo leo wakati alipowatembelea
wanajeshi wa nchi hiyo katika mji wa Baga kaskazini mwa jimbo la Borno
huko kaskazini mashariki mwa Nigeria. Jeshi la Nigeria lilisema tarehe
21 mwezi huu kuwa, limeukomboa mji wa Baga kutoka mikononi mwa
wanamgambo wa Boko Haram ambao waliuteka mji huo tarehe 3 mwezi Januari
mwaka huu baada ya siku mbili za mapigano.Mkuu wa jeshi la Nigeria amesema vita karibu vimekwisha na kwamba jeshi hilo litaikomboa miji ya Dikwa, Bama, Gwoza, Marte na maeneo mengine ya Nigeria siku chache zijazo. Jeshi la Nigeria limeyasema hayo huku nchi jirani na Nigeria zikifanya juhudi za kurejesha amani huko Nigeria kabla ya kufanyika uchaguzi mkuu nchini humo tarehe 28 mwezi ujao.



0 comments:
Post a Comment