Kenya kuanzia leo inakuwa mwenyeji wa
mkutano wa 16 wa Marais wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Mkutano
huo ambao unaanza shughuli zake leo utafanyika katika kituo cha KICC
jijini Nairobi. Pamoja na mambo mengine, mkutano wa 16 wa Marais wa nchi
za Jumuiya ya Afrika Mashariki utajadili pia ripoti ya kila mwaka ya
baraza la mawaziri katika kipindi cha kati ya mwezi Disemba mwaka juzi
hadi Novemba mwaka jana.
Mkutano huo pia utatupia jicho ripoti ya
maendeleo katika utekelezaji wa maamuzi makuu yaliyosalia ambayo ni
muhimu kwa jumuiya hiyo. Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) inatazamiwa
pia kupata Mwenyekiti mpya. Kiti cha uwenyekiti wa jumuiya hiyo hivi
sasa kinashikiliwa na Kenya. Suala la kuwateuwa majaji wa Mahakama ya
Haki ya Afrika Mashariki pia litakuwa katika ajenda ya mkutano huo.



0 comments:
Post a Comment