Katibu mkuu wa zamani wa umoja wa
mataifa Kofi Annan amewasili nchini Cuba kuhamasisha mazungumzo ya amani
kati ya serikali ya Colombia na nchi zenye makundi ya waasi.Hata hivyo katika mazungumzo hayo ya Amani lengo ni kumaliza migogoro iliyodumu kwa zaidi ya miongo mitano.
Annan amesema atakutana na pande zote mbili za viongozi na kuwa na mazungumzo nao ya pamoja na kwamba atatumia uzoefu wake wa utatuzi wa migogoro katika nchi alizowahi kuwa msuluhishi.



0 comments:
Post a Comment