Serikali ya Liberia imeahidi kufungua
mipaka yake na nchi jirani kuanzia kesho Jumapili. Aidha Rais Ellen
Johnson Sirleaf wa nchi hiyo amekubaliana na pendekezo la kufunguliwa
vivuko vya mipaka ya nchi hiyo ambavyo vilifungwa mwaka jana kwa lengo
la kuzuia maambukizi ya ugonjwa hatari wa Ebola sambamba na kutangaza
kufutwa amri ya kutotoka nje. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, hatua hiyo
itatekelezwa kuanzia kesho tarehe 22 Februari. Virusi vya ugonjwa hatari
wa Ebola vilienea kwa kasi sana mwaka jana 2014 katika nchi za Guinea
Conakry, Sierra Leone na Liberia na kupelekea maelfu ya watu kupoteza
maisha huku makumi ya maelfu ya wengine wakiwa wameambukizwa maradhi
hayo. Hayo yanajiri katika hali ambayo hivi karibuni serikali ya Sierra
Leone iliziwekea karantini zaidi ya nyumba 700 katika mji mkuu wa nchi
hiyo Freetown, baada ya mtu mmoja kufariki dunia kwa ugonjwa huo. Kwa
mujibu wa ripoti za mashirika ya afya, maambukizi ya ugonjwa huo
yamepungua sana, suala linaloleta matumaini ya kumalizika kabisa Ebola
huko magharibi mwa Afrika.Liberia sasa kufungua mipaka yake baada ya Ebola

huko magharibi mwa Afrika.

0 comments:
Post a Comment