Kwa mara ya kwanza Rais Robert Gabriel
Mugabe wa Zimbabwe amekiri makosa yake kuhusiana na suala la ardhi
lililozua mjadala mkubwa nchini humo mwaka 2000. Taarifa kutoka Harare,
mji mkuu wa nchi hiyo zimemnukuu Rais Mugabe akizungumza kupitia
televisheni ya taifa kwamba ardhi walizogawiwa watu weusi raia wa nchi
hiyo, ni kubwa sana na kwamba hawawezi kuzisimamia. Mugabe ameongeza
kuwa, licha ya raia hao kupatiwa ardhi kubwa, lakini wengi wao wameweza
kulima theluthi moja tu ya ardhi hizo. Matamshi hayo ya Rais Mugabe
mwenye umri wa miaka 91 yanatajwa kuwa ya kwanza kutolewa na kiongozi
huyo. Kwa miaka 10 sasa Zimbabwe ambayo ilikuwa moja ya wazalishaji wa
chakula barani Afrika, imegeuka na kuwa nchi waagizaji chakula kutoka
nje. Zaidi ya walowezi 4000 wa Ulaya waliokuwa wamehodhi ardhi kubwa za
kilimo nchini humo, walilazimishwa kuondoka na ardhi hizo kupewa wenyeji
wa Zimbabwe. Nchi za Ulaya zililalamikia vikali marekebisho hayo ya
ardhi huko Zimbabwe ambapo baadhi ya wachambuzi wa mambo wanaamini Rais
Mugabe alitumia suala hilo kwa maslahi ya kisiasa.Mugabe: Siasa za ardhi Zimbabwe hazikuwa sahihi

Mugabe alitumia suala hilo kwa maslahi ya kisiasa.

0 comments:
Post a Comment