Serikali ya Mali imekubali kusitisha uhasama na Waasi wa Tuareg kaskazini mwa Nchi hiyo.Makubaliano hayo ni sehemu ya mazungumzo yanayoendelea ya kurejesha hali ya utulivu kaskazini mwa Mali, miaka miwili baada ya Jeshi la Ufaransa kuwafurusha Waasi wa kiislamu.
Lakini kumekuwa na wasiwasi kuwa bado itakuwa vigumu kupata suluhu hasa kwa mambo kama ya kukabidhi Madaraka kaskazini mwa Mali ambapo Waasi wanaita Azawad.



0 comments:
Post a Comment