Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania imetoa taarifa rasmi kuhusu uhalifu uliotikisa mkoani Tanga,
ikisema hali ni shwari na umma wa Watanzania upuuze taarifa
zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zikitia hofu. Kaimu Kamanda wa
Polisi wa Mkoa wa Tanga, Juma Ndaki amesema kuwa, watu kadhaa
wanashikiliwa wakihusishwa na uhalifu huo. Akitoa taarifa kwa waandishi
wa habari, Kamanda Ndaki amesema hali katika kitongoji cha Majimoto,
Amboni na mkoa wa Tanga kwa ujumla iko shwari na kwamba, wanaendelea
kufanya uchunguzi kubaini hao wahalifu pamoja na silaha zilizoibiwa.
Amesema, wanaomba wananchi waendelee kutoa ushirikiano wao hasa
wanapoona watu wenye majeraha au wanaowahisi kwamba ni wahalifu ili
waweze kuwachunguza kama wanahusika kwenye tukio hilo. Kwa upande wake
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Magalula Said Magalula aliwataka wakazi wa Tanga
na vitongoji vyake, kuondoa hofu kwa kuhakikisha wanaendelea na shughuli
zao za uzalishaji kwa sababu ulinzi umeimarishwa na hali ya usalama ni
shwari. Pia, aliwataka wananchi na wageni wenye mpango wa kutembelea
eneo la kihistoria la Mapango ya Amboni, kuendelea na ratiba zao kwa
sababu eneo hilo liko salama na tangu awali halikuhusika kwenye vurugu
hizo.'Tanga ni shwari baada ya uhalifu uliotikisa mkoa huo'

hizo.

0 comments:
Post a Comment