Aliyekuwa rais wa Uturuki Kenan
Evren ambaye aliongoza mapindunzi yaliyokumbwa na umwagikaji wa damu
mwaka 1980 ameaga dunia kwenye hospitali moja mjini Ankara akiwa na umri
wa miaka 97.Chini ya utawala wake watu kadha walinyongwa , maelfu wakakamatwa na vyama vya kisiasa vikapigwa marufuku.
Vyombo vya habari vilivyotangaza kinyume na mapinduzi hayo vilifungwa . Generali Evren alidai kuwa alileta udhabiti nchini Uturuki.



0 comments:
Post a Comment