Rais
Barack Obama ameliambia kongamano dhidi ya misimamo mikali ya kidini
akisema kuwa kuwa wako kwenye vita si na Waislamu bali na magaidi
waliouchafua Uislamu.Bwana Obama amesema ni sharti dunia
ikabiliane na itikadi zilizopindishwa na makundi kama Islamic State
yanayochochea vita na kuwapa vijana mafundisho yenye misimamo mikali ya
imani ya kidini .
Ameyasema hayo katika mkutano wa siku tatu
unaofanyika mjini Washington ambapo amesema dunia inatakiwa kukabiliana
na makundi ya aina hiyo.
Rais Obama ameeleza kuwa manung'uniko
waliyonayo vijana lazima yashughulikiwe ili kuondokana na hisia za
makundi yenye misimamo mikali ya kiitikadi.
Wawakilishi kutoka
zaidi ya nchi sitini wanahudhuria mkutano huo ambao umekuja kufuatia
mashambulio ya makundi ya Kiislam katika nchi za Denmark, Ufaransa na
Australia.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment