Uongozi wa muziki nchini marekani
unao muongoza msanii wa R&B Chris Brown umetoa taarifa kwa uongozi
wa muziki Tanzania unao muongoza msanii kutoka Tanzania ALI KIBA msanii
ambae yupo chini ya uongozi wa Kampuni za SAMSUNG...>>>>
Kwa taarifa zilizopo katika mtandao
wa VIP Beats nchini marekani zinaeleza kua tarehe 24 mwezi wa 11 mwaka
2014 uongozi wa msanii Chris Brown ulipokea maombi ya muungano wa
wasanii wawili kufanya wimbo wa pamoja kati ya msanii Ali kiba na Chris
Brown maombi hayo yaliambatanishwa na Softcopy zilizobeba nyimbo tatu za
msanii Ali kiba ikiwemo SINGLE BOY, MWANA pamoja na wimbo aliofanya
katika project ya ONE 8.
Uongozi wa Chris Brown
umethibitisha kupokea taarifa za maombi hayo na umeonesha kupenda sauti
ya msanii Ali kiba na kutoa tamko kua wapo tayari kusimamia kazi ya
pamoja itakayofanywa na wasanii hawa.
Upande wa msanii Chris Brown
amesema hana tatizo yupo tayari kushirikiana na msanii Ali kiba kwani
alipata nafasi ya kutazama project ya One 8 na ameona kiwango cha msanii
Ali kiba kinaridhisha japokua anahitaji marekebisho madogo sana.
BBC SWAHILI Tunampongeza msanii Ali
kiba kwa juhudi zake tunamtakia kila lakheri katika kazi hii, kuipata
habari hii kamili tembelea mtandao wa VIP Beats, Channel 0 au unaweza
kuipata katika American Spring news.
0 comments:
Post a Comment