Magaidi wa kitakfiri wa kundi la Boko Haram nchini Nigeria
wamewaua kwa umati wakaazi wa mji wa Gwoza waliokuwa wamekusanyika
kusoma Qur'ani Tukufu kaskazini mashariki mwa nchi hiyo. Wakaazi wa mji
huo wamenukuliwa wakisema kuwa katika jinai hiyo ya Jumanne iliyopita,
magaidi waliwaua kwa umati watu wasiopungua 68 wengi wao wakiwa vijana
na watoto waliokuwa wamekusanyika katika kikao cha kusoma Qu'rani.
Mashuhuda wanasema Boko Haram walitumia silaha mpya kabisa katika
kuzingira kikao hicho cha kusoma Qur'ani Tukufu na wakawafyatulia risasi
kiholela waliokuwa hapo. Seneta wa eneo hilo Ali Nduwe amenukuliwa
akisema kuwa magaidi wa Boko Haram waliuvamia mji huo wa Gwoza siku
chache zilizopita na kuwaua wanaume huku wanawake na watoto wakilazimika
kuyakimbia makazi yao.Huku hayo yakijiri kinara wa Boko Haram ametangaza utiifu wake kwa kundi la kigaidi la Daesh (ISIL). Abubakr Shekau ametangaza kupitia mtandao wa kijamii wa twitter kuwa anamtii kiongozi wa kundi la kitakfiri la Daesh, Abubakr Baghdad. Katika siku za hivi karibuni magaidi wa Boko Haram wamekuwa wakitekeza jinai na ukatili sawa na ule wa kundi la Daesh kama vile kuwachinja na kuwateketeza moto watu wasio na hatia.



0 comments:
Post a Comment