Utafiti uliofanywa na timu ya wachunguzi wa kimataifa umeonyesha
kuwa maradhi ya Ebola katika nchi za Guinea Conakry, Liberia na Sierra
Leone yameanika udhaifu ulioko katika sekta za afya za nchi hizo.
Watafiti hao wa kimataifa wamesema nchi hizo za Magharibi mwa Afrika
zimeshindwa kuwekeza ipasavyo katika sekta ya afya na hivyo kupelekea
ugonjwa wa Ebola kusababisha maafa makubwa. Kukosekana vituo vya afya na
madaktari wa kutosha katika nchi hizo ni moja ya sababu zilizoashiriwa
kwenye ripoti ya uchunguzi ya watafiti kutoka shirika la madaktari wasio
na mipaka MSF.Takwimu za Shirika la Afya duniani (WHO) zinaonyesha kuwa takriban watu 10 000 wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa wa Ebola tangu uliporipuka magharibi mwa Afrika mwaka 2013.



0 comments:
Post a Comment