Gazeti moja la Kizayuni limearifu kuwa utawala wa Kizayuni wa
Israel umefanya mashambulizi ya anga huko Sudan. Gazeti la Kizayuni la
Maariv limezinukuu duru za Sudan na kuandika kuwa, ndege za Israel kwa
mara nyingine tena zimeishambulia Sudan. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, duru
za Sudan zimetangaza kuwa sauti za milipuko zilisikika jana usiku huko
Khartoum mji mkuu wa nchi hiyo kufuatia mashambulizi ya anga ya utawala
wa Kizayuni wa Israel.Baadhi ya duru za Kiarabu pia zimetangaza kuwa mashambulizi hayo yalikusudiwa kukilenga kituo kimoja cha kuundia silaha. Wakati huo huo viongozi wa Sudan wameashiria rekodi ya mashambulizi ya huko nyuma ya Israel dhidi ya nchi hiyo na kuunyooshea kidole cha tuhuma moja kwa moja utawala huo ghasibu.



0 comments:
Post a Comment