Kocha wa Chelsea Jose Mourinho
amesema kwamba haoni uongozi wa alama 7 juu ya jedwali la ligi ya
Uingereza ni fursa ya timu hiyo kushinda ligi hiyo mwaka huu.
The
Blues iliishinda Aston Villa 2-1 siku ya jumamosi huku Manchester City
Inayoshikilia nafasi ya pili katika jedwali hilo ikiangukia sare ya 1-1
dhidi ya Hull City.James Milner alifunga bao la Mancity lakini hakuisaidia timu yake kupunguza pengo lililopo kati yake na Chelsea katika uongozi wa Ligi.
Everton na Liverpool nazo zilitoka sare ya 0-0 katika Merseyside Derby iliochezwa katika uwanja wa Goodison Park
Haya hapa baadhi ya matokeo ya mechi zilizochezwa jumamosi.
Aston Villa 1 - 2 Chelsea
Leicester 0 - 1 Crystal Palace
Man City 1 - 1 Hull
QPR 0 - 1 Southampton
Swansea 1 - 1 Sunderland
Everton 0 - 0 Liverpool
0 comments:
Post a Comment