
Ripoti mpya inasema kuwa Wasomali
milioni 3 wanaotegemea kuhamisha fedha kutoka ng'ambo wako katika hatari
ya kukabiliwa na njaa iwapo njia zao za kupata fedha zitafungwa.
Onyo
hilo linajiri wiki mbili tu baada benki ya Marekani Merchants Bank of
California ambayo imekuwa ikishughulikia uhamishaji wa fedha kwa 80%
kutoka Marekani hadi Somalia kufunga huduma zake kutokana na wasiwasi
kuwa fedha hizo zilikuwa zinawafikia wapiganaji wa Al-Shabaab.
Mwaka
uliopita Benki ya Barclays nchini Uingereza ilifunga huduma ya
kusafirisha pesa katika akaunti za Somali na benki za Australia vile
vile zinafikiria kuchukua hatua ama hiyo.
About
NELSON PASCHAL KAMUGISHA
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment