Miaka 27 iliyopita katika siku
kama ya leo, inayosadifiana na tarehe Mosi Esfand 1366 Hijria Shamsia,
ndege moja ya abiria ya Iran ilishambuliwa na kutunguliwa kwa kombora la
majeshi ya utawala wa kidikteta wa Saddam Hussein wa Iraq na
kuangushwa, wakati wa vita vya Iran na Iraq. Katika tukio hilo,
Hujjatulislam Fadhlullah Mahallati, mwakilishi wa Imam Khomeini kwenye
Kikosi cha Kulinda Mapinduzi ya Kiislamu (Sepah) aliuawa shahidi akiwa
pamoja na viongozi na wabunge 39 wa Iran.
Siku kama ya leo miaka 68
iliyopita, inayosadifiana na tarehe 20 Februari 1947, Uingereza hatimaye
ilikubali kuipatia India uhuru wake baada ya kuikoloni nchi hiyo kwa
karne mbili. Uhuru wa India ulipatikana kutokana na mapambano ya muda
mrefu yaliyoongozwa na Mahatma Gandhi. Katika kipindi chote cha utawala
wake wa kikoloni huko India, Uingereza ilipora utajiri na maliasili ya
nchi hiyo na kuwasababishia hasara kubwa raia wa India. Mwezi Agosti
mwaka huohuo India na Pakistan zilitengana na kuwa nchi mbili.
Na miaka 225 iliyopita siku
kama ya leo yaani mwaka 1211 Hijiria, alifariki dunia mshairi mkubwa wa
Kiislamu Sheikh Kadhim Tamimi Baghdadi, maarufu kwa jina la Azri akiwa
na umri wa miaka 80. Alikuwa msomi na mwafasihi mkubwa na ameacha diwani
ya mashairi. Miongoni mwa mshairi ya malenga huyu maarufu wa Kiislamu
ni shairi maarufu la "Al Azriya" ambalo linamsifu Mtukufu Mtume Muhammad
(saw) na kizazi chake kitukufu na kubainisha misingi ya dini ya
Uislamu. Shairi hilo lina zaidi ya beti 1000.
0 comments:
Post a Comment