Mapigano makali yameendelea mashariki mwa Ukraine kufuatia majeshi ya
serikali kukabiliana na kundi la Waasi wanaodaiwa kuungwa mkono na
Urusi.
Raia wanane na wanajeshi wanne wameuawa kufuatia mashambulizi ya
silaha kati ya majeshi ya serikali na Waasi katika mji wa Kramatorsk
unaoshikiliwa na serikali.
Hata hivyo mapigano hayo yanakuja huku
kukiwa na mpango wa mazungumzo ya amani ili kusitisha mapigano hayo.
Vyombo vya habari nchini Urusi vinasema makubaliano ya muda ya
kusimamisha mapigano yamefikiwa, japo kuwa hakuna uthibitisho wa
serikali. Mapambano bado yanaendelea katika mji wa Debaltseve na
wanajeshi wa serikali wa Ukraine wamefanya mashambulizi dhidi ya waasi
mashariki mwa Mariupol.
About
NELSON PASCHAL KAMUGISHA
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment