
Ndege za kivita za Nigeria jana
zilizishambulia kambi za mafunzo, maficho ya silaha na magari ya
wanamgambo wa kundi la Boko Haram katika msitu wa kaskazini mashariki wa
Samibisa. Msemaji wa jeshi la Nigeria Meja Jenerali Chris Olukolade
amesema kuwa wanamgambo wengi wa kundi la Boko Haram wameuliwa kwenye
mashambuliz hayo huku wengine wakikimbilia katika maeneo mbalimbali ya
msitu na nje ya kambi zao za mafunzo zilizoshambuliwa.
Baada ya kupita mwaka mmoja ambapo
wanamgambo wa Boko Haram wameonekana kusonga mbele huku wakiteka maeneo
mengi, kuua maelfu ya watu na kuwateka nyara mamia ya wengine, wengi
wakiwa ni wanawake na watoto, hali ya mambo ilionekana kuwageukia mwezi
uliopita, baada ya nchi kadhaa jirani na Nigeria kuamua kuanzisha
mashambulizi dhidi ya kundi hilo. Vikosi vya Nigeria vimetangaza kuwa
vimewauwa wanamgambo wa Boko Haram zaidi ya 300 katika oparesheni
iliyofanywa na jeshi hilo ya kuikomboa miji na vijiji 11 tangu mwanzoni
mwa wiki hii.
About
NELSON PASCHAL KAMUGISHA
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment