Fainali za kombe la dunia kwa mwaka
2022 nchini Qatar huenda sasa zitafanyika mwezi Novemba na Desemba hiyo
ni kwa mujibu wa Mkuu wa jopo kazi ya shirikisho la kandanda duniani
Sheikh Salman Bin
Ebrahim amesema mapendekezo ilikuwa iwe mwezi May lakini wakati huo utakuwa vigumu kwani ni majira ya joto.Duru zinaeleza kuwa wakati huo kiwango cha joto nchin humo hutimia nyuzijoto 40huku viwango vya joto katika msimu wa baridi ukitimia nyuzijoto kati ya 20 na 30.
Aidha ratiba hiyo ya awali inatarajiwakugongana na fainali za michuano fainali za Klabu Bingwa barani Ulaya.
Mapendekezo hayo yanatarajiwa kupitishwa katika kongamano la wajumbe wa FIFA huko Zurich juma lijalo.
Sheikh Salman bin Ebrahim Al-Khalifa aliyeongoza jopokazi hilo anasema kuwa kamati yake vilevile imependekeza kupunguzwa kwa siku za kuandaliwa kwa mechi hizo.
Mapendekezo ya kamati hiyo inatarajiwa kukabiliwa na upinzani mkubwa haswa kutoka kwa viongozi wa kanda ya ulaya ambao wanatarajiwa kusema kuwa ratiba hiyo ya kombe la dunia itahitilafiana na ligi zao.
Nchi ya Qatar ilipewa jukumu la kuandaa mashindano hayo mwaka 2022 lakini imebainika kuwa fainali hizo zitagongana na majira ya joto kali katika eneo hilo,la ghuba jambo ambalo ni kikwazo wa afya za wachezaji.
Mapendekezo mengine yalikuwa iwe kati ya mwezi Januari au Februari lakini imeonekana zitagongana na mashindano ya Olympic.
Hassan Al Thawad mkuu wa kamati ya maandalizi ya finali hizo nchini Qatar ameiambia BBC kuwa Qatar imekubaliana na mapendekezo ya kamati ya shirikisho la kandanda duniani Fifa.
0 comments:
Post a Comment