Shirika la habari la Xinhua limemnukuu msemaji wa jeshi la Kenya akilionya kundi hilo kutokana na vitisho vyake vya kufanya mashambulizi ndani ya Kenya na katika nchi za Magharibi. David Obonyo pia amesema kuwa, vikosi vya ulinzi vya Kenya vimechukua hatua muhimu za kiusalama baada ya kundi la ash Shabab la Somalia kusambaza mkanda wa video wakitishia kufanya mashambulizi mengine ya kigaidi nchini Kenya. Amesema, kundi la ash Shabab limekasirika kutokana na kukombolewa miji ya kiistratijia nchini Somalia kufuatia mashambulizi makubwa ya anga ya jeshi la Kenya kwenye ngome za kundi hilo. Siku ya Jumamosi, kundi la ash Shabab la Somalia lilisambaza mkanda wa video likitishia kufanya mashambulizi katika maeneo ya biashara kweye nchi za Kenya, Canada, Uingereza na Marekani. Kwa upande wake, msemaji wa jeshi la polisi la Kenya, (Kitengo cha Utawala) Masoud Mwinyi, amesisitiza kuwa, hatua za usalama zimeimarishwa nchini humo na kuwataka raia wa nchi hiyo kuchukua tahadhari wanapokuwepo kwenye maeneo ya biashara. Serikali ya Kenya iko katika mashinikizo yalipotokea uvamizi wa kigaidi katika kituo cha biashara cha Westgate jijini Nairobi mwezi Septemba 2013. Uvamizi huo ulipelekea watu 67 kuuawa.
Jeshi la Kenya lawaonya wanamgambo wa al- Shabab

0 comments:
Post a Comment