
Kocha wa Chelsea Jose Mourinho
hakuweza kuhimili presha kama mkufunzi wa Real Madrid ,aliyekuwa rais wa
kilabu hiyo Ramon Calderon amesema.
Mkufunzi huyo wa Chelsea
aliifunza kilabu hiyo kutoka mwaka 2010 hadi mwaka 2013, na hivyobasi
kushinda taji la La Liga mwaka 2012 na taji la Copa Del Rey mwaka 2011
kabla ya kuelekea Stamford Bridge.
''Kuwa Meneja wa kilabu ya Real
Madrid sio mchezo ni vigumu sana'',Calderon aliiambia BBC. Angalia
kilichompata Mourinho.''Ni mtu ambaye hakuweza kuhimili presha'',.
Mourinho
alimaliza wa pili katika La Liga katika msimu wake wa pili kama
mkufunzi wa Real Madrid,ikiwa ni alama nne nyuma ya Barcelona,lakini
alishinda ligi mwaka uliofuata alipoipatia Real Madrid pointi 100.
About
NELSON PASCHAL KAMUGISHA
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment