TENGENEZA BLOG BOMBA SASA..

LEO KATIKA HISTORIA Jumamosi, Februari 21

https://renegadeexpression.files.wordpress.com/2013/07/malcolm-x.jpgLeo ni Jumamosi tarehe Pili Mfunguo Nane Jamad al-Awwal 1436 Hijria mwafaka na tarehe 21 Februari mwaka 2015 Miladia.
Siku kama ya leo miaka 50 iliyopita, Malcolm X, Mmarekani mweusi aliuawa baada ya kushambuliwa na magaidi. Malcolm X alizaliwa mwaka 1925, na wakati alipokuwa kwenye rika la ujana alifahamiana na makundi ya vijana wa Kiislamu na hatimaye akasilimu. Itikadi ya mwanaharakati huyo wa Kiislamu iliwachukiza watawala wa Marekani na makundi ya ubaguzi wa rangi nchini humo. Malcolm X aliuawa wakati akihutubia mkutano. Alikuwa akisisitiza mara kwa mara kwamba, Wamarekani wenye asili ya Afrika ambao wanakandamizwa na kubaguliwa na serikali ya Marekani wanaweza kujipatia uhuru na uadilifu chini ya mwamvuli wa sheria za Kiislamu. ***
Katika siku kama ya leo miaka 57 iliyopita, wananchi wengi wa Misri na Syria walishiriki kwenye kura ya maoni ya kuunganisha nchi mbili hizo chini ya Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu. Wananchi hao walimchagua Gamal Abdul-Nasser, kiongozi wa wakati huo wa Misri, kuwa Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Kiarabu. Baada miezi kadhaa, Yemen nayo ilijiunga na muungano huo. Hata hivyo muungano huo haukudumu kwa zaidi ya miaka mitatu, kwani Syria ilitangaza kujitoa kwenye muungano huo baada ya kutoridhishwa na uongozi wa Gamal Abdul-Nasser. ***
Miaka 99 iliyopita katika siku kama ya leo, vilianza vita vikali vya umwagaji damu vilivyojulikana kwa jina la Verdun kati ya Ujerumani na Ufaransa. Vita hivyo vilivyodumu kwa muda wa miezi kumi vilimalizika kwa kushindwa vikosi vya Ujerumani. Kushindwa huko kulikuwa moja ya sababu ya kushindwa baadaye Ujerumani kwenye Vita vya Kwanza vya Dunia.***
Na katika siku kama ya miaka 1023 iliyopita kulingana na kalenda ya Hijria, aliaga dunia Abul Hassan Ali bin Hilal Baghdadi mashuhuri kwa jina la Ibn al-Bawwab, mwanafasihi na msomi aliyekuwa amebobea katika fani ya hati. Alisifika mno kwa kuwa na hati nzuri na aliweza kuweka sheria na kanuni mpya katika sanaa ya hati. Abul Hassan Ali bin Hilal Baghdadi au Ibn al- Bawwab kama anavyojulikana pia ameacha nakala nyingi zenye hati nzuri na za kuvutia za Qur'ani Tukufu ambazo zimehifadhiwa nchini Uingereza.***
Share on Google Plus

About NELSON PASCHAL KAMUGISHA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

CREATED AND DESIGNED BY NELLYPAKA(WWW.NELLYPAKA.BLOGSPOT.COM)