TENGENEZA BLOG BOMBA SASA..

'Tanga ni shwari baada ya uhalifu uliotikisa mkoa huo'

'Tanga ni shwari baada ya uhalifu uliotikisa mkoa huo' Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoa taarifa rasmi kuhusu uhalifu uliotikisa mkoani Tanga, ikisema hali ni shwari na umma wa Watanzania upuuze taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zikitia hofu. Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Juma Ndaki amesema kuwa, watu kadhaa wanashikiliwa wakihusishwa na uhalifu huo. Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari, Kamanda Ndaki amesema hali katika kitongoji cha Majimoto, Amboni na mkoa wa Tanga kwa ujumla iko shwari na kwamba, wanaendelea kufanya uchunguzi kubaini hao wahalifu pamoja na silaha zilizoibiwa. Amesema, wanaomba wananchi waendelee kutoa ushirikiano wao hasa wanapoona watu wenye majeraha au wanaowahisi kwamba ni wahalifu ili waweze kuwachunguza kama wanahusika kwenye tukio hilo. Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Magalula Said Magalula aliwataka wakazi wa Tanga na vitongoji vyake, kuondoa hofu kwa kuhakikisha wanaendelea na shughuli zao za uzalishaji kwa sababu ulinzi umeimarishwa na hali ya usalama ni shwari. Pia, aliwataka wananchi na wageni wenye mpango wa kutembelea eneo la kihistoria la Mapango ya Amboni, kuendelea na ratiba zao kwa sababu eneo hilo liko salama na tangu awali halikuhusika kwenye vurugu hizo.
Share on Google Plus

About NELSON PASCHAL KAMUGISHA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

CREATED AND DESIGNED BY NELLYPAKA(WWW.NELLYPAKA.BLOGSPOT.COM)