Rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo ametangaza kujiengua kutoka chama tawala cha nchi hiyo cha People's Democratic (PDP). Hayo yanajiri katika hali ambayo zimebakia wiki sita kuelekea uchaguzi mkuu wa nchi wa rais. Jana mchana Obasanjo alitangaza kujiondoa rasmi katika chama hicho, na kuichana hadharani kadi ya uanachama wake. Siku mbili kabla rais huyo wa zamani wa Nigeria alitangaza kuwa, Rais Goodluck Jonathan, anafanya njama za kila aina kuhakikisha anaendelea kubakia madarakani. Olusegun Obasanjo mwenye umri wa miaka 77 na aliyewahi kuhudumu kama jenerali jeshini, aliliongoza taifa la Nigeria mwaka 1970, na baada ya nchi hiyo kurejea kwenye mfumo wa kidemokrasia mwaka 1999, akaiongoza tena nchi hiyo kwa mihula miwili. Inaelezwa kwamba, uungaji mkono wa Obasanjo kwa Jonathan ulipelekea rais huyo wa hivi sasa wa Nigeria kushinda katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2011, hata hivyo uhusiano wa wawili hao umeharibika katika miaka ya hivi karibuni. Aidha hivi karibuni, Obasanjo alitangaza azma yake ya kumuunga mkono Muhammad Buhari, mpinzani mkuu wa Jonathan katika uchaguzi wa tarehe 28 mwezi Machi mwaka huu. Weledi wa mambo wameitaja hatua ya kujiondoka katika chama tawala mwanasiasa mkubwa huyo kwamba itapelekea uchaguzi wa mwaka huu, kuwa na mchuano mkubwa.
Obasanjo ajiengua chama tawala nchini Nigeria

0 comments:
Post a Comment