
Mwendesha mashtaka wa Burundi ametangaza kuwa, watu kadhaa wanaoshukiwa
kuhusika na mauaji ya Jenerali Adolph Nshimirimana wamekamatwa. Jenerali
huyo alikuwa mpambe wa Rais Pierre Nkurunziza na aliuawa kwenye
shambulizi la roketi dhidi ya gari lake wiki iliyopita. Taarifa kutoka
ofisi ya mwendesha mashtaka imesema kuwa, waratibu wakuu wa mauaji hayo
bado wanasakwa lakini tayari watu kadhaa wanaoaminika kutekeleza jinai
hiyo wametiwa mbaroni. Msemaji wa polisi ya Burundi, Pierre Nkurikiye
amethibitisha kukamatwa washukiwa hao ingawa hakutoa maelezo zaidi. Rais
Pierre Nkurunziza alikuwa ameipa polisi ya Burundi wiki moja
kukamilisha uchunguzi na kuwakamata wahusika wa mauaji ya Jenerali
Adolph Nshimirimana. Kuna hofu kwamba huenda polisi wamewakamata watu
ambao si wahusika ili kumuonyesha rais kuwa wanafanya kazi kwa mujibu wa
matarajio ya ikul
About
NELSON PASCHAL KAMUGISHA
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment