Manchester United
wamemuulizia 'kimyakimya' mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane, 22 na
watafanya maombi rasmi iwapo Spurs watakubali (Daily Mirror), Manchester
City wanaamini kuwa watakamilisha uhamisho wa kiungo wa Wolfsburg Kevin
De Bryne, 24 kabla hawajacheza na Chelsea siku ya Jumapili (Daily
Mail), Chelsea wataongeza dau lao la pauni milioni 30 kumtaka beki wa
kati John Stones, 21, kutoka Everton (Daily Mirror), meneja wa Everton
Roberto Martinez amesema Stones ni "professional" ambaye "hatozira"
iwapo uhamisho wake kwenda Chelsea hautafanikiwa (Guardian), West Ham
watawapa Manchester United pauni milioni 12 kumsajili Javier Hernandez
baada ya kukataliwa dau la mwanzo la pauni milioni 8 (Daily Star), beki
wa kushoto wa Everton Leighton Baines, 30, huenda asicheze kwa miezi
mitatu baada ya kufanyiwa upasuaji wa mguu wiki hii (Daily Express),
kipa wa Manchester United David De Gea amesema alikuwa tayari kucheza
dhidi ya Tottenham siku ya Jumamosi, licha ya Louis van Gaal kudai kuwa
hakuwa tayari kutokana na tetesi za kuhamia Real Madrid (Daily Mail),
meneja wa Manchester City Manuel Pellegrini anaamini Raheem Sterling
anaweza kufika thamani ya pauni milioni 100 siku za usoni (Manchester
Evening News), Pellegrini amekiri kuwa kazi yake itakuwa mashakani kama
hatoshinda Ligi Kuu msimu huu (Sun), beki kutoka Argentina Martin
Demichelis, 33, anaamini Manchester City wana nafasi kubwa ya kushinda
ligi msimu huu (Sky Sports), meneja wa Arsenal, Arsene Wenger amekataa
kumrushia lawama kipa Petr Cech, 33, kwa jinsi alivyocheza katika mechi
waliyopoteza 2-0 dhidi ya West Ham (Daily Star), meneja wa zamani wa
Tottenham na QPR Harry Redknapp anaamini kuwa Arsenal wanaweza kushinda
ligi licha ya kupoteza mechi ya kwanza, lakini ikiwa watasajili
mshambuliaji mwingine (Daily Telegraph). Tetesi nyingine kesho
tukijaaliwa. Share hizi na wapenda soka.
EPL leo usiku
EPL leo usiku

0 comments:
Post a Comment