TENGENEZA BLOG BOMBA SASA..

TETESI ZA SOKA ULAYA IJUMAA 08.08.2015



Matumaini ya Manchester United kumsajili beki wa Real Madrid, Sergio Ramos, 29, yamefufuka tena baada ya beki huyo kukasirishwa na Real kusitasita kumlipa pauni 135,000 anazotaka kwa wiki (AS), Manchester United wenyewe wanasita kutoa pauni milioni 23 kutengua kifungu cha uhamisho cha mshambuliaji wa Barcelona Pedro 28. Old Trafford wanasema wanadhani mchezaji huyo ana thamani ya pauni milioni 17 (Daily Mirror), Arsenal bado wana uhakika wa kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzima, 27, licha ya Arsene Wenger kutupilia mbali tetesi hizo (Daily Star), uhamisho wa Emmanuel Adebayor kutoka Tottenham kwenda Aston Villa unaonekana kukwama baada ya mchezaji huyo kugoma kuhamia "mikoani" (Birmingham Mail), Villa pia huenda wakamkosa beki Joleon Lescott, huku West Brom wakiwa tayari kumpa mkataba mchezaji huyo (Mirror), beki wa kati wa Atletico Madrid amekataa mkataba wa pauni 88,000 kwa wiki kuhamia Manchester City (Marca), beki wa Inter Milan Danilo D'Ambrosio, 26 ameshindwa kukubaliana maslahi binafsi ya West Ham baada ya timu hizo mbili kukubaliana uhamisho wa pauni milioni 9 (Talksport), West Ham wamepata kibali cha kufanya kazi kinachotakiwa kumuwezesha mshambuliaji wa Atletico Madrid Raul Jiminez, 24 kusajiliwa kwa mkopo (Daily Mail), West Ham pia wamemuuliza mshambuliaji wa Liverpool Fabio Borini, 24, lakini mchezji huyo huenda akahamia Fiorentina (Times), Everton na Tottenham wanamyatia kiungo kutoka Japan Keisuke Honda, 29, baada ya AC Milan kuamuua kumuuza (Tuttosport), West Brom wanakaribia kumsajili kiungo wa Arsenal Serge Gnabry, 20 kwa mkopo (Talksport). Habari zilizothibitishwa nitakujuza. Uwe na siku njema-- Cheers!!
Share on Google Plus

About NELSON PASCHAL KAMUGISHA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

CREATED AND DESIGNED BY NELLYPAKA(WWW.NELLYPAKA.BLOGSPOT.COM)