
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya Jumamosi ya leo ameanza ziara ya siku tatu
katika nchi jirani ya Uganda. Katika safari yake hiyo Rais Kenyatta
anatarajiwa kukutana na mwenyeji wake Rais Yoweri Museveni ambapo
viongozi hao wanatarajiwa kufanya mazungumzo kuhusiana na uhusiano wa
pande mbili na masuala ya kibiashara.
Marais hao wanatarajiwa pia
kubadilishana mawazo kuhusiana na hali ya Sudan Kusini na vilevile hali
ya mambo nchini Burundi ambapo Rais Museveni ni mpatanishi wa Jumuiya ya
Afrika Mashariki katika mgogoro wa kisiasa nchini humo.
Akiwa nchini
Uganda Rais Kenyatta mbali na kukutana na jumuiya ya wafanyabiasha wa
Uganda atakutana pia na Wakenya wanaoishi nchini humo. Taarifa zaidi
zinasema siku ya Jumatatu Rais wa Kenya anatarajiwa kulihutubia Bunge la
Uganda.
About
NELSON PASCHAL KAMUGISHA
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment