Tottenham wako tayari kumnyatia mshambuliaji wa QPR Charlie Austin, 26, ambaye atagharimu karibu pauni milioni 15 (Daily Mirror), Spurs pia wanatarajia kuwazidi kete PSV na Atletico Madrid katika kumsajili winga kutoka Colombia Jeison Lucumi, 20, anayechezea America de Cali ya daraja la pili (Daily Mail), mshambuliaji mpya wa Manchester United Memphis Depay, 21, amemuambia meneja Louis van Gaal kuwa anataka kuvaa jezi namba 7 aliyokuwa akivaa Angel Di Maria (Telegraph), nahodha wa Chelsea John Terry anaamini Chelsea itakuwa timu ya kwanza kutetea taji lake mfululizo katika kipindi cha miaka saba (Evening Standard), Real Madrid wanaweza kushawishiwa kumuuza Karim Benzima, 27, lakini Arsenal watalazimika kuvunja rekodi yao ya uhamisho kwa kutoa pauni milioni 45 (Daily Mail), Asier Illarramendi, 25, ameambiwa na Real Madrid kuwa hana nafsi ya kucheza katika klabu hiyo msimu huu na hivyo huenda akafikiria kuhamia Liverpool (Daily Express), Liverpool wanazungumza na Fiorentina kuhusu uhamisho wa Fabio Borini, 24 (Talksport), Angel Di Maria anatarajia kutangazwa rasmi kwa mashabiki wa Paris Saint-Germain leo (Daily Star), beki wa kushoto wa Augsburg Baba Rahman, 21, amekubali kuhamia Chelsea, lakini bado timu hizo mbili hazijakubaliana bei (Sky Sports), Manchester United wamepanda dau jingine kumtaka mshambuliaji wa Tottenham Harry Kane (Daily Express), Nigeria imefanya juhudi za kumshawishi nyota chipukizi wa Liverpool Jordon Ibe, 19, kuichezea timu ya taifa ya Nigeria, badala ya England ambayo ameichezea katika ngazi ya vijana (Daily Mirror), Sergio Aguero, David Silva na Samir Nasri, huenda wakakosa mechi za mwanzo wa msimu baada ya kurejeshwa nyumbani kutoka mazoezini wakisumbuliwa na tatizo la tumbo (Daily Star), mshambuliaji wa zamani wa Liverpool El Hadji Diof, 34, ambaye anaichezea klabu iitwayo Saba ya Malaysia amesema anataka kuingia katika siasa atakapostaafu soka (Sun), uhamisho wa mkopo wa kiungo Leroy Fer wa QPR kwenda Sunderald umeshindikana baada ya mchezaji huyo kutopita vipimo vya afya (Independent), Saido Berahino huenda akasalia kuwa mchezaji wa West Brom, baada ya klabu hiyo kusema haijasikia lolote kutoka kwa Tottenham waliokuwa wakimnyatia (Birmingham Mail), mshambuliaji wa Manchester United Javier Hernandez amepewa dau la dola milioni 10 na klabu moja ya ligi ya Marekani MLS, na amepewa saa 24 kuamua hatma yake (NBC Sports).na Lionel Messi ameonekana kama akimpiga 'kichwa' beki wa Roma katika mechi ya kirafiki ambayo Barcelona ilishinda 3-0 kwenye uwanja wa Nou Camp. Mshambuliaji huyo kutoka Argentina, 28, alioneshwa kadi ya manjano kwa tukio hilo, ambapo pia alimkaba koo Mapou Yanga-Mbiwa. Messi ambaye hajawahi kuoneshwa kadi nyekundu akiichezea Barcelona, -- alionekana akijibu mapigo baada ya wachezaji hao wawili 'kutunishiana misuli'. Messi alipata bao katika mchezo huo. Barcelona wanaanza msimu wao kwa kupambana na Athletic Bilbao Agosti 23. Beki wa zamani wa Newcastle, Yanga-Mbiwa pia alioneshwa kadi ya manjano huku wachezaji wenzao wakijaribu kuwaamua. Kadi nyekundu pekee ya Messi ilikuwa wakati akiichezea Argentina kwa mara ya kwanza, dakika mbili baada ya kuingia kama mchezaji wa akiba wakati Argentina ikicheza na Hungary.
MSIMAMO WA FIFA
Msimamo wa timu za taifa, wa Fifa mwezi huu umetoka. Argentina imeendelea kusalia kileleni, Ubelgiji imeingia nafasi ya pili, na kuishusha Ujerumani hadi nafasi ya tatu. Kwa timu za Afrika Mashariki- Uganda imeshuka nafasi moja hadi namba 74, Rwanda imeporomoka nafasi 13 hadi namba 91, Kenya imesalia palepale namba 116, Burundi imeshuka nafasi moja hadi namba 132, na Tanzania nayo kudondoka nafasi moja hadi 140.
Msimamo kamili wa mataifa yoye unaweza kuuona kupitia link hii:
http://www.fifa.com/fifa-world-ranking/ranking-table/men/
Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Share tetesi hizi na wapenda soka wote. Cheers!!
0 comments:
Post a Comment