Manchester United wameambiwa wasahau kumsajili Harry Kane, 22, huku Tottenham wakisisitiza kuwa hawatomuuza mshambuliaji huyo (Guardian), United huenda wakaweza kumsajili mshambuliaji wa Barcelona Pedro, 29, ambaye alipachika bao la ushindi katika mechi ya Supercopa, na amedaiwa kusema anataka kuondoka (Times), meneja wa Arsenal Arsene Wenger anafikiria kutoa pauni milioni 22 kumtaka kiungo wa Sevilla Grzegorz Krychowiak, 25 (Daily Telegraph), Manchester City wamemtaka Kevin De Bryne kutamka wazi kuwa anataka kuondoka (Manchester Evening News), Chelsea wanajiandaa kumsajili beki wa kushoto Abdul Rahman Baba, 21, kwa pauni milioni 17 (Sun), Sunderland watajaribu kumsajili winga wa Manchester United Adnaj Januzaj, 20, (Sunderland Echo), West Ham wameacha kumfuatilia kiungo wa zamani wa QPR Joey Burton, 32, baada ya mashabiki kumkataa (MIrror), Torino wanataka kumsajili mshambuliaji wa Manchester United Javier Hernandez, 27 kwa mkopo na baadaye moja kwa moja (Mirror), Schalke wamesema dau "kubwa sana" ndio litaweza kuwashawishi kumuuza kiungo wao Julian Drexler, 21 ambaye ananyatiwa na Arsenal na Manchester United (Daily Star), Aston Villa wanakaribia kumsajili winga kutoka Barcelona Adama Traore, 19, kwa pauni milioni 12 (Daily Mail), meneja wa Chelsea Jose Mourinho anasita kumuachia kiungo kutoka Brazil, Ramires, 28 kuondoka huku akinyatiwa na Juventus (London Evening Standard), QPR watampta mkataba mpya mshambuliaji wao Charlie Austin iwapo hakuna atakayeweza kumnunua kwa pauni milioni 15 (London Evening Standard).Na
Mshambuliaji wa Manchester City, Edin Dzeko amejiunga na AS Roma ya Italia. Manchester City wamesema ni kwa mkopo kwa sasa na utakuwa usajili wa kudumu iwapo "masuala kadhaa" yatafikiwa.
Mshambuliaji kutoka Uruguay, anayeichezea Barcelona, Luis Suarez, ametajwa katika orodha ya wachezaji watatu wanaowania tuzo ya UEFA ya mchezaji bora wa Ulaya. Suarez anaungana na mshambuliaji mwenzake wa Barcelona Lionel Messi na vilevile katika orodha hiyo yuko hasimu wake Messi, Cristiano Ronaldo. Messi na Ronaldo walifunga mabao 77. UEFA wamesema wachezaji hawa watatu walipata kura nyingi zilizopigwa na waandishi wa habari kutoka katika orodha ya wachezaji kumi. Waandishi hao wa habari wapatao 54 ndio watamchagua mshindi wa tuzo hii ya mwaka 2014-15, tarehe 27 Agosti mjini Monaco. Siku hiyo pia ni ya droo ya Klabu Bingwa Ulaya.
![](https://fbcdn-sphotos-c-a.akamaihd.net/hphotos-ak-xfp1/v/t1.0-9/11026280_639358042868328_736225399417751236_n.jpg?oh=a5a908830c886444002160e0039a8535&oe=56844B14&__gda__=1447643791_0576fa999ac68c357813529dee134539)
Share tetesi hizi na wapenda soka wote.
0 comments:
Post a Comment