Mshambuliaji wa Liverpool
Mario Balotelli, 25, atakataa kujiunga na Lazio au Sampdoria kwa mkopo
kwa sababu atalipwa fedha nyingi tu za 'uzalendo' kama bado atakuwepo
Anfield dirisha la uhamisho likifungwa (Daily Mirror), Juventus
wanafikiria kumchukua kiungo wa Liverpool Lucas, 28, ambaye hakutajwa
kwenye kikosi cha Brendan Rodgers dhidi ya Stoke wiki iliyopita (Daily
Express), matumaini ya Manchester United kumsajili beki wa Real Madrid
Sergio Ramos, 29, yamekwisha baada ya beki huyo kujiandaa kuongeza
mkataba wake wiki ijayo (Guardian),meneja wa Manchester United Louis van
Gaal amesema ana matumaini kuwa mshambuliaji Wayne Rooney, 29, ataweza
kupachika mabao zaidi ya 20 msimu huu (Independent), mshambuliaji wa
Tottenham, Roberto Soldado, 30, amesafiki kwenda Spain kukamilisha
uhamisho wake kwenda Villareal (Guardian), Emmanuel Adebayos, 31, wa
Tottenham na Javier Hernandez wa Manchester United, 27, ni kati ya
washambuliaji wanaonyatiwa na West Ham (London Evening Standard),
Everton wanamtaka beki wa zamani wa kushoto wa Manchester United
Alexander Buttner, 26, kuziba nafasi ya Leighton Baines aliyeumia (Daily
Mail), Fifa imemshutumu meneja wa Chelsea Jose Mourinho kwa jinsi
alivyofarakana na daktari wa timu Dr Eva Carneiro (Daily Telegraph),
Sunderland wamekuwa na mazungumzo ya kumsajili tena mshambuliaji Fabio
Borini kwa mkopo, mwaka mmoja baada ya mchezaji huyo kukataa kwenda
Stadium of Light (Sunderland Echo), QPR wanakaribia kumsajili beki wa
Bolton Tim Ream, 27 (NBC Sports). NA TURUDI KWA Mourinho

Bi Carneiro aliingia uwanjani katika muda wa lala salama kumtibu kiungo wa Chelsea Eden Hazard ambaye alionekana kagongwa kifundo cha mguu.
'The special one' alisema kuwa daktari mkuu Carneiro na msaidizi wake Fearn hawatakuwa uwanjani Chelsea itakapokuwa ikipambana na Manchester City siku ya jumapili.

''Hii haimaanishi kuwa hawatakuwepo siku nyingine ,katika siku za usoni'' alisema Mourinho.
Kocha huyo aliyasema hayo baada ya kukutana na kitengo kizima cha utabibu cha Chelsea siku ya Alhamisi.
Carneiro aliwakilishwa katika mkutano huo na mawakili wake kutoka kwa kampuni ya mawakili ya Mishcon de Reya

Mourinho aliwataja Carneiro na Fearn kuwa 'wajinga' baada yao kuingia uwanjani kumtibu Hazard katika dakika za lala salama ya mechi ya kufungua msimu.
Kutokana na shinikizo la wapinzani wao Mourinho aliona kuwa kumuondoa Hazard katika kipindi hicho kuliwasaidia wapinzani wao kuwa na wachezaji wawili zaidi hivyo kuwazidi nguvu,

Mourinho alipoulizwa iwapo anauhusiano mzuri na na kitengo hicho cha utabibu alisema kuwa
''Mimi nao tunahusiana kama kawaida tu vile ''

'Wenyewe wamenieleza kuwa hawajawahi kushabikiwa zaidi ya kipindi hichi nilipoingia Chelsea''
''Walinieleza kuwa wanahitaji kukosolewa ili na wao wajiendeleze''
Share hizi na wapenda soka wote.
Mourinho:Daktari'mjinga' hatakuwepo uwanjan
Meneja wa Chelsea manager Jose Mourinho amekariri msimamo wake dhidi ya kitengo cha utabibu cha timu yake.
Mourinho
aliwakaripia Dakta Eva Carneiro na Jon Fearn kwa kuingia uwanjani huku
timu hiyo ikisalia na wachezaji wachache kufuatia kufurushwa kwa kipa
nambari moja Thibaut Courtois katika mechi ngumu ya kufungua msimu kati
yao na Swansea Bi Carneiro aliingia uwanjani katika muda wa lala salama kumtibu kiungo wa Chelsea Eden Hazard ambaye alionekana kagongwa kifundo cha mguu.
'The special one' alisema kuwa daktari mkuu Carneiro na msaidizi wake Fearn hawatakuwa uwanjani Chelsea itakapokuwa ikipambana na Manchester City siku ya jumapili.
''Hii haimaanishi kuwa hawatakuwepo siku nyingine ,katika siku za usoni'' alisema Mourinho.
Kocha huyo aliyasema hayo baada ya kukutana na kitengo kizima cha utabibu cha Chelsea siku ya Alhamisi.
Carneiro aliwakilishwa katika mkutano huo na mawakili wake kutoka kwa kampuni ya mawakili ya Mishcon de Reya
Mourinho aliwataja Carneiro na Fearn kuwa 'wajinga' baada yao kuingia uwanjani kumtibu Hazard katika dakika za lala salama ya mechi ya kufungua msimu.
Kutokana na shinikizo la wapinzani wao Mourinho aliona kuwa kumuondoa Hazard katika kipindi hicho kuliwasaidia wapinzani wao kuwa na wachezaji wawili zaidi hivyo kuwazidi nguvu,
Mourinho alipoulizwa iwapo anauhusiano mzuri na na kitengo hicho cha utabibu alisema kuwa
''Mimi nao tunahusiana kama kawaida tu vile ''
'Wenyewe wamenieleza kuwa hawajawahi kushabikiwa zaidi ya kipindi hichi nilipoingia Chelsea''
''Walinieleza kuwa wanahitaji kukosolewa ili na wao wajiendeleze''
Share hizi na wapenda soka wote.
0 comments:
Post a Comment