TENGENEZA BLOG BOMBA SASA..

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMATATU 17.08.2015

Real Madrid watampa David De Gea, 24, pauni milioni 24 kama ada ya usajili, iwapo atamalizia mkataba wake ulosalia wa mwaka mmoja Old Trafford, wakati atakapoondoka bure msimu ujao (Daily Mirror), Manchester City wanakaribia kukamilisha usajili wa pauni milioni 28.5 wa beki wa Valencia Nicolas Otamendi, 27, huku Eliaquim Mangala, 24, akitarajiwa kwenda Spain kwa mkopo (Daily Mail), Manchester City wataongeza dau lao la pauni milioni 43 kumtaka kiungo wa Wolfsburg, Kevin De Bruyne (Sky Sports), Tottenham wapo tayari wiki hii kutoa dau la pauni milioni 15 kumtaka mshambuliaji wa West Brom, Saido Berahino, 22, huku beki Joleon Lescott, 33, kiungo Stephane Ssesegnon, 31, Brown Ideye, 26 na Victor Anichebe pia wakiruhusiwa kuondoka (Telegraph), dau la pauni milioni 5 kutoka Chelsea kumtaka beki wa Galatasaray Alex Telles limekataliwa (Daily Star), Everton watamnyatia beki wa Swansea Ashley Williams, 30, iwapo John Stones, 21, atakwenda Chelsea (Daily Star), meneja wa Everton Roberto Martinez pia anataka kumsajili mshambuliaji wa Dynamo Kiev Andriy Yarmolenko (Liverpool Echo), meneja wa West Ham Slaven Bilic anamtaka kipa wa QPR Robert Green, 35, akitaka kuimarisha makipa wake (Sun), Newcastle na Everton wanamtaka beki Jannik Vestegaard, 23, wa Werder Bremen, lakini beki huyo anasema hana habari (Daily Express). . Na


 KWINGINEKO KATIKA SOKA

  "Sikuwahi kutaka kuondoka" asema Ramos
Beki wa Real Madrid Sergio Ramos amesema hakuwahi kutaka kuondoka Bernabeu, licha ya taarifa kadhaa kumhusisha na kuhamia Manchester United. Ramos, ambaye amesaini mkataba wa miaka mitano amesema: "Wazo langu lilikuwa kubakia hapa na kustaafu hapa kama rais angeruhusu hilo, na na ninashukuru sasa nina changamoto mpya ya kuwa nahodha wa timu hii.
"Sikuwahi kusema nataka kuondoka, nilikuwa kimya. Sikusema chochote kutokana na kuheshimu wachezaji wenzangu na rais, sikuwahi kupiga simu kwenye ofisi yetu na kutaka fedha zaidi."
 Real Madrid defender Sergio Ramos with club president Florentino Perez



 Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa

Share on Google Plus

About NELSON PASCHAL KAMUGISHA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

CREATED AND DESIGNED BY NELLYPAKA(WWW.NELLYPAKA.BLOGSPOT.COM)