Matamshi yaliyotolewa na
kiungo Kevin De Bryne, 24 kuwa atabakia Wolfsburg msimu ujao yamepuuzwa
na wakala wake na hivyo kuwepo bado na uwezekano wa uhamisho wa pauni
milioni 50 kwenda Manchester City (Times), Chelsea wametoa dau jingine
jipya la pauni milioni 30 kumtaka beki John Stones, 21, lakini huenda
fedha hizo zikaongezeka kwa pauni milioni 10 zaidi ili kufanikisha
uhamisho huo kutoka Everton (Telegraph), meneja wa Chelsea pia atapewa
fedha zaidi na Roman Abramovich kununua wachezaji wengine wawili kabla
dirisha la uhamisho halijafungwa kufuatia kuanza vibaya msimu mpya
(Daily Mirror), Everton watamwania, ama- Ashely Williams, 30, wa Swansea
au Kalidou Koulibaly, 24 wa Napoli, iwapo Stones ataondoka Goodison
Park (Daily Star), Arsenal na Manchester United wametaarifiwa uwepo wa
Zlatan Ibrahimovic, 33, ambaye ameambiwa na klabu yake ya PSG kuwa
anaweza kuondoka kwa bei nafuu (Daily Mail), Manchester City wameambiwa
waongeze dau kama wanamtaka beki wa Valencia Nicolas Otamendi (Sky
Sports), City hawatomruhusu Eliaquim Mangala, 24, kwenda Valencia kama
sehemu ya mkataba wa kumsajili Otamendi (Daily Express), mkurugenzi mkuu
wa Manchester United Ed Woodward amekwenda Barcelona kujaribu
kukamilisha uhamisho wa Perdo (Daily Mail), Newcastle wameacha
kumfuatilia mshambuliaji wa QPR Charlie Austin kutokana na bei yake ya
pauni milioni 15 (Newcastle Chronicle), hata hivyo West Ham bado
wanataka kumsajili Austin (Evening Standard), Newcastle wanakaribia
kumsajili winga wa Marseille Florian Thauvin, 22, katika mkataba ambao
Remy Cabella, 25, atakwenda Ufaransa (Guardian), Juventus huenda
wakamsajili Eric Lamela, 23, kutoka Tottenham iwapo watashindwa
kumsajili Christian Eriksen, 23 (Evening Standard), Sunderland wanataka
kumrejesha tena mchezaji kiraka wa Aston Villa Kieran Richardson, 30
(Daily Mirror), Southampton wanakaribia kukamilisha usajili wa beki wa
Napoli Kalidou Koulibaly, 24 kwa pauni milioni 8.5 na bado pia wanamtaka
beki wa kati wa Celtic Virgil van Dijk (Daily Star), Sunderland wana
wasiwasi watashindwa kumsajili Fabio Borini wa Liverpool na watazidiwa
kete na Inter Milan (Sunderland Echo), West Brom wamepanda dau la pauni
milioni 5 kumtaka Federico Fazio wa Tottenham (Telegraph), Norwich
wanataka kumsajili Mattia Destro kwa mkopo kutoka Roma (Times), kipa wa
Manchester United atatafakari kumfukuza kazi wakala wake Jorge Mendes
iwapo hatofanikisha uhamisho wake kwenda Real Madrid kabla ya dirisha la
usajili kufungwa (Independent).
NA MATOKE YA LEO NI KAMA

NA MATOKE YA LEO NI KAMA

0 comments:
Post a Comment