
Chelsea watajaribu kuwazidi
kete Manchester United katika kumsajili mshambuliaji wa Barcelona
Pedro, 28 (Mail), Chelsea watafikiria kuongeza dau na kufikia pauni
milioni 40 kumsajili beki wa Everton John Stones, 21, baada ya dau la
pauni milioni 30 kukataliwa (Guardian),Fernabahce watamshawishi beki wa
Chelsea John Terry na mshahara wa pauni milioni 2.5 kwa mwaka ili ahamia
Uturuki (Mail), Branislav Ivanovic, 31, huenda akawekwa bench
na
Jose Mourinho baada ya Chelsea kumsajili Abdul Baba Rahman ambaye
anaweza kuanza siku ya jumapili dhidi ya West Brom (Mirror), Manchester
City watakamilisha usajili wa pauni milioni 88 kwa beki wa Valencia
Nicolas Otamendi na Kevin De Bryce (Mirror), West Brom wamewaambia
Tottenham kuwa watahitaji kutoa pauni milioni 25 kumsajili Saido
Berahino, 22 (Independent), Bournemouth wanataka kumsajili mshambuliaji
wa Sunderland Jermain Defoe, 32, ambaye aliwahi kuichezea klabu hiyo
akiwa bado kijana (Mirror), Arsenal watahitaji kulipa pauni milioni 35
kama wanataka kumsajili mshambuliaji wa PSG Edinson Cavani (Eurosport),
Real Madrid wana matumaini kuwa wanaweza kumtumia kipa Keylor Navas, 28,
katika jitihada zao za kutaka kumsajili kipa wa Manchester United David
De Gea, 24 (Marca), rais wa AC Milan Silvio Berlusconi amemwambia
mshambuliaji wa PSG Zlatan Ibrahimovic, 33, kuwa anasubiriwa kwa "moyo
mkunjufu" kurejea San Siro (Gazzetta World). NA
Manchester United wanajaribu kumsajili winga wa Southampton Sadio Mane.
Dau la kumtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa Senegal, 23 liliwasilishwa
wiki iliyopita. Mshambuliaji wa Barcelona, Perdo, alikuwa akinyatiwa na
United, lakini sasa anakaribia kujiunga na Chelsea kwa pauni milioni 21.
Mane alipachika mabao 10 katika mechi 32 msimu uliopita baada ya
kujiunga na Southampton akitokea Red Bull Salzburg. Mane pia alipachika
"Hat Trick" ya haraka zaidi katika historia ya Ligi Kuu ya England.
Beki wa kati wa Barcelona, Gerard Pique amefungiwa kucheza mechi nne
baada ya kuoneshwa kadi nyekundu kwa kumtukana mwamuzi wa pembeni kwenye
mchezo wa Super Cup dhidi ya Athletic Bilbao siku ya Jumatatu.
Barcelona wanaweza kukata rufaa, na adhabu hiyo kupunguzwa, lakini
ikikataliwa, mchezaji huyo wa kimataifa wa Spain atakosa mechi nne za
mwanzo za La Liga. Pique aliomba radhi kwa kupewa kadi nyekundu siku na
Jumanne, lakini anakanusha kutumia lugha chafu.
About
NELSON PASCHAL KAMUGISHA
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment