
Benjamin William Mkapa Rais mstaafu wa Tanzania amesema kuwa, sekta ya
uwekezaji nchini humo inashindwa kukua kwa kasi kama inayotarajiwa
kutokana na baadhi ya wanasiasa kushindwa kuielewa vizuri. Akizungumza
wakati wa kusaini makubaliano ya kusaidia kuvutia na kuongeza uwekezaji
wa ndani na nje nchini kati ya Taasisi inayoshughulikia Mazingira ya
Uwekezaji Barani Afrika ICF na Kituo cha Uwekezaji nchini Tanzania TIC,
Mkapa ambaye pia ni Mwenyekiti mwenza wa ICF alisema kuwa, baadhi ya
watu wanautazama uwekezaji kama unyonyaji. Chini ya makubaliano hayo,
ICF itakisaidia kituo cha uwekezaji nchini katika kukuza, kuinua na
kulitangaza dirisha la uwekezaji na kuimarisha uwezo wake katika
kuwezesha na kufuatilia uwekezaji nchini Tanzania. Naye Mwenyekiti
mwenza wa ICF Neville Isdell alisema kuwa, uwekezaji unahitaji uwazi ili
kuwavutia wafanyabiashara wa ndani na nje kuendelea kuwekeza.
About
NELSON PASCHAL KAMUGISHA
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment