TENGENEZA BLOG BOMBA SASA..

TETESI ZA SOKA ULAYA JUMANNE 11.08.2015

 
 
Manchester City wametoa dau la pili la pauni milioni 47 kumtaka winga wa Wolfsburg, Kevin De Bryne, 24 katika jitihada zao za kusajili mchezaji wa tano msimu huu (Guardian), Everton watakataa dau la pauni milioni 30 kutoka Chelsea la kumtaka beki John Stones, 20 (Daily Mail), hata hivyo Everton wanafikiria kumfuata beki wa AC Milan Cristian Zapata, 28, kuziba nafasi ya Stones iwapo ataondoka (ESPN), Real Madrid wamewasilisha dau la mwisho la pauni milioni 21 kumtaka kipa wa Manchester United David De Gea, 24 (ABC), Stoke watamsajili kiungo wa Inter Milan Xherdan Shaqiri, 23 kwa pauni milioni 12 (Sun), Tottenham wamezidisha nia yao ya kumtaka mshambuliaji wa Manchester United Javier Hernandez, 27 pamoja na Saido Berahino, 21, na wana uhakika wa kumpata japo mshambuliaji mmoja katika dirisha hili (London Evening Standard), Spurs pia wana matumaini ya kukamilisha usajili wa mshambuliaji kutoka Cameroon, Clinton N'Jie kutoka Lyon (Daily Telegraph), Tottenham pia wana nafasi kubwa ya kumsajili mshambuliaji wa FC Basel, Breel Embolo kwa pauni milioni 10 (Daily Mirror), Liverpool wapo tayari kupokea dau kwa kiungo wao mkongwe Lucas Leiva, 28 (Liverpool Echo), Manchester United wamefikia makubaliano na beki kutoka Argentina Lucas Biliga, 29, na watamsajili kwa pauni milioni 17.7 kutoka Lazio (Le10Sport), matumaini ya Manchester United kumsajili Sergio Ramos yamefifia tena baada ya beki huyo kushawishiwa na mkataba mpya wenye marupurupu yanayofikia pauni milioni 7.1 kwa mwaka (London Evening Standard), West Brom wanajiandaa kumsajili beki kutoka Spain Jose Enrique, 29 (Tuttomercatoweb), Everton huenda wanakaribia kumsajili beki wa Manchester United Jonny Evans, 27 (Metro), Chelsea wanakaribia kumsajili beki wa kushoto Baba Rahman, 21 katika mkataba utakaofikia pauni milioni 21.7 (Daily Express). Tetesi nyingine kesho tukijaaliwa. Na 
 Rufaa ya Chelsea kupinga kadi nyekundu aliyooneshwa kipa Thibault Courtois katika mchezo dhidi ya Swansea, siku ya Jumamosi, imetupiliwa mbali na Chama cha Soka cha England, FA.
Courtois sasa atakosa mechi ya Jumapili dhidi ya Manchester City
 

Share on Google Plus

About NELSON PASCHAL KAMUGISHA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

CREATED AND DESIGNED BY NELLYPAKA(WWW.NELLYPAKA.BLOGSPOT.COM)