Mashirika kadhaa ya kutetea haki za binaadamu nchini Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Kongo zimeikosoa
serikali ya nchi hiyo kwa kuwafunga
wanaharakati wa haki za binaadamu. Zaidi ya taasisi 30 za kutetea haki
za binaadamu nchini humo mapema leo zimeikosoa serikali hiyo kwa
kuendelea kumshikilia korokoroni Christopher Ngoy Mutamba, mwanaharakati
wa haki za binaadamu aliyetiwa mbaroni tarehe 21 mwezi Januari mwaka
huu. Aidha mashirika hayo yameonyesha wasi wasi wao kuhusiana na
kukosekana uadilifu katika uendeshaji wa kesi ya mtuhumiwa huyo.
Wasiwasi huo umekuja kufuatia mahakama moja ya nchi hiyo kutangaza
kuendelea kumshikilia Mutamba kwa muda zaidi. Mutamba alitiwa mbaroni
tarehe 21 katika machafuko yaliyopelekea watu 42 kuuawa na mamia ya
wengine kutiwa mbaroni na polisi ya nchi hiyo. maandamano hayo yaliibuka
kupinga mpango wa mabadilisho ya kuendelea kusalia madarakani Rais
Joseph Kabila wa nchi hiyo.
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment