TENGENEZA BLOG BOMBA SASA..

Liberia sasa kufungua mipaka yake baada ya Ebola

Liberia sasa kufungua mipaka yake baada ya Ebola Serikali ya Liberia imeahidi kufungua mipaka yake na nchi jirani kuanzia kesho Jumapili. Aidha Rais Ellen Johnson Sirleaf wa nchi hiyo amekubaliana na pendekezo la kufunguliwa vivuko vya mipaka ya nchi hiyo ambavyo vilifungwa mwaka jana kwa lengo la kuzuia maambukizi ya ugonjwa hatari wa Ebola sambamba na kutangaza kufutwa amri ya kutotoka nje. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, hatua hiyo itatekelezwa kuanzia kesho tarehe 22 Februari. Virusi vya ugonjwa hatari wa Ebola vilienea kwa kasi sana mwaka jana 2014 katika nchi za Guinea Conakry, Sierra Leone na Liberia na kupelekea maelfu ya watu kupoteza maisha huku makumi ya maelfu ya wengine wakiwa wameambukizwa maradhi hayo. Hayo yanajiri katika hali ambayo hivi karibuni serikali ya Sierra Leone iliziwekea karantini zaidi ya nyumba 700 katika mji mkuu wa nchi hiyo Freetown, baada ya mtu mmoja kufariki dunia kwa ugonjwa huo. Kwa mujibu wa ripoti za mashirika ya afya, maambukizi ya ugonjwa huo yamepungua sana, suala linaloleta matumaini ya kumalizika kabisa Ebola huko magharibi mwa Afrika.
Share on Google Plus

About NELSON PASCHAL KAMUGISHA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

CREATED AND DESIGNED BY NELLYPAKA(WWW.NELLYPAKA.BLOGSPOT.COM)