Siku kama ya leo miaka 9 iliyopita, inayosadifiana na 22
Februari 2006, Haram mbili takatifu za Maimamu al Hadi na Hassan
al-Askari katika mji wa Samarra nchini Iraq, ziliharibiwa vibaya kwenye
mashambulizi kadhaa ya miripuko ya mabomu yaliyofanywa na makundi ya
kigaidi na kupelekea hasara kubwa za mali na watu. Maimamu hao ni
wajukuu wa Mtume Bwana Mtume Muhammad SAW, na waliokuwa na nafasi kubwa
ya kielimu na uchaji-Mungu katika zama zao. Kitendo cha kuharibiwa eneo
hilo kiliwakasirisha mno Waislamu duniani hususan wafuasi wa Ahlul Bait
wa Mtume (saw). Nukta ya kufaa kukumbusha ni kwamba, kabla ya kujiri
mashambulizi hayo, ulinzi wa haramu hizo, ulikuwa kwa majeshi vamizi ya
Marekani. Shambulio hilo lilifanyika kwa lengo la kuzusha ufa kati ya
safu za Waislamu wa madhehebu za Shia na Suni nchini Iraq.
Siku kama ya leo miaka 57 iliyopita, inayosadifiana na 22
Februari 1958, Abul-Kalaam Ahmad Azad, msomi, khatibu na mwanasiasa wa
India alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 70. Abul Kalaam Azad alinza
harakati za kisiasa akiwa na umri wa miaka 17 dhidi ya utawala wa
kikoloni wa Uingereza kwa shabaha ya kuwazindua Waislamu wa India. Msomi
huyo aliwekwa gerezani mara kadhaa na wakoloni kutokana na hatua zake
za kuchapisha na kutoa hotuba zenye kufichua ukandamizaji wa Uingereza.
Baada ya India kuwa huru, alichaguliwa kuwa mbunge na Waziri wa Elimu wa
nchi hiyo.
Siku kama ya leo miaka 97 iliyopita, Mirza Swadiq Hakim,
maarufu kwa jina la Adibul-Mamaalik Farahani, alifariki dunia. Akiwa
kijana mdogo, Mirza alisoma elimu mbalimbali na fasaha ya lugha ya
Kifarsi na lugha nyengine za Ulaya. Kwa miaka yote Adibul-Mamaalik,
alijishughulisha na uandishi sanjari na kusimamia idara za magazeti ya
lugha na shughuli nyengine za kiserikali. Mbali na hayo msomi huyo
alitabahari pia katika uwanja wa mashairi kwa kufuata nyendo za watalamu
wa zamani wa mashairi.
Na siku kama ya leo, miaka 144 iliyopita, alifariki dunia
Ayatullah Mirza Abu Abdillah, Sheikhul-Islami Zanjani, msomi mkubwa na
mshairi wa Kiislamu. Msomi huyo mkubwa, alizaliwa mwaka 1224 Hijiria
mjini Zanjani, moja ya miji ya Iran na kuelekea mjini Isfahani kwa ajili
ya masomo akiwa kijana mdogo. Akiwa Isfaham Ayatullah Mirza Abu
Abdillah alipata kusoma katika hauza ya kielimu ambayo ilikuwa na
itibari kubwa kielimu wakati huo. Baada ya kuhitimu masomo yake alirejea
eneo alikozaliwa na kujishughulisha na kuwalea wanafanzu wake.
0 comments:
Post a Comment