TENGENEZA BLOG BOMBA SASA..

Kenya mwenyeji wa mkutano wa 16 wa EAC

Kenya mwenyeji wa mkutano wa 16 wa  EAC Kenya kuanzia leo inakuwa mwenyeji wa mkutano wa 16 wa Marais wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Mkutano huo ambao unaanza shughuli zake leo utafanyika katika kituo cha KICC jijini Nairobi. Pamoja na mambo mengine, mkutano wa 16 wa Marais wa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki utajadili pia ripoti ya kila mwaka ya baraza la mawaziri katika kipindi cha kati ya mwezi Disemba mwaka juzi hadi Novemba mwaka jana.
Mkutano huo pia utatupia jicho ripoti ya maendeleo katika utekelezaji wa maamuzi makuu yaliyosalia ambayo ni muhimu kwa jumuiya hiyo. Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) inatazamiwa pia kupata Mwenyekiti mpya. Kiti cha uwenyekiti wa jumuiya hiyo hivi sasa kinashikiliwa na Kenya. Suala la kuwateuwa majaji wa Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki pia litakuwa katika ajenda ya mkutano huo.
Share on Google Plus

About NELSON PASCHAL KAMUGISHA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

CREATED AND DESIGNED BY NELLYPAKA(WWW.NELLYPAKA.BLOGSPOT.COM)