Washiriki wa maandamano hayo
wamesisitiza sualal la kuwepo amani na maelewano kati ya wafuasi wa dini
mbalimbali na kupinga hatua zenye kuchochea chuki za kidini na vitendo
vya ukatili kwa jina la dini vinavyojiri katika maeneo mbalimbali.
Mwakilishi wa Waislamu katika maandamano hayo ya London amesisitiza kuwa
wafuasi wa dini mbalimbali wanataka amani, kuishi kwa maelewano na
kuheshimiana kila mmoja. Maandamano ya amani ya mjini London ambayo ni
jibu kwa mashambulizi ya hivi karibuni katika miji ya Paris na
Copenhagen, yameandaliwa na kundi la viongozi wa kidini wa Uingereza
chini ya anuani" mpango wa kuishi kwa amani kati ya wafuasi wa dini
mbalimbali."
- Blogger Comment
- Facebook Comment
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
0 comments:
Post a Comment