TENGENEZA BLOG BOMBA SASA..

Ebola yaanika udhaifu wa sekta ya afya A/Magharibi

Ebola yaanika udhaifu wa sekta ya afya A/MagharibiUtafiti uliofanywa na timu ya wachunguzi wa kimataifa umeonyesha kuwa maradhi ya Ebola katika nchi za Guinea Conakry, Liberia na Sierra Leone yameanika udhaifu ulioko katika sekta za afya za nchi hizo. Watafiti hao wa kimataifa wamesema nchi hizo za Magharibi mwa Afrika zimeshindwa kuwekeza ipasavyo katika sekta ya afya na hivyo kupelekea ugonjwa wa Ebola kusababisha maafa makubwa. Kukosekana vituo vya afya na madaktari wa kutosha katika nchi hizo ni moja ya sababu zilizoashiriwa kwenye ripoti ya uchunguzi ya watafiti kutoka shirika la madaktari wasio na mipaka MSF.
Takwimu za Shirika la Afya duniani (WHO) zinaonyesha kuwa takriban watu 10 000 wamepoteza maisha kutokana na ugonjwa wa Ebola tangu uliporipuka magharibi mwa Afrika mwaka 2013.

Share on Google Plus

About NELSON PASCHAL KAMUGISHA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

CREATED AND DESIGNED BY NELLYPAKA(WWW.NELLYPAKA.BLOGSPOT.COM)