TENGENEZA BLOG BOMBA SASA..

Mahakama ya ICC yamuondolea tuhuma Rais wa Kenya

Mahakama ya ICC yamuondolea tuhuma Rais wa Kenya  Majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) ya The Hague Uholanzi leo wametoa taarifa na kutangaza uamuzi wao wa kufuta tuhuma dhidi ya  Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya.
Weledi wa mambo wameutaja uamuzi huo wa mahakama ya ICC kuwa ni kufeli kukubwa zaidi kwa taasisi hiyo ya kimataifa tangu kuundwa kwake. Wakati huo huo weledi hao wamekutathmini kufungwa faili la kesi ya Uhuru Kenyatta na kufutiwa tuhuma za kuhusika katika machafuko ya baada ya uchaguzi wa Rais wa mwaka 2007, kuwa ni mafanikio makubwa kwa kiongozi huyo wa Kenya.
Uhuru Kenyatta ni Rais wa kwanza duniani aliyemadarakani kuwahi kushtakiwa katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) kwa tuhuma za kutenda jinai dhidi ya binadamu na kuamuru machafuko ya umwagaji damu nchini kwake. Mchuano mkali uliokuwepo kati ya Mwai Kibaki na Raila Odinga Rais na Waziri Mkuu wa wakati huo wa Kenya, katika uchaguzi wa mwezi Disemba mwaka 2007 ulikuwa wa aina yake na haujawahi kushuhudiwa katika siasa za nchi hiyo ya mashariki mwa Afrika. Kama ilivyo katika nchi nyingi za kusini mwa jangwa la Sahara, katika kipindi kifupi tu mapigano kati ya watu wa makabila mawili hasimu ya Kikuyu na Kalenjin yalibadilika na kuwa mvutano mkubwa wa kikabila na kisiasa. Mivutano hiyo ya kikabila na kisiasa iliyoendelea hadi mwanzoni mwa mwaka 2008, ilisababisha mauaji ya karibu watu 1133 na Wakenya wengine 650,000 wakalazimika kukimbia nyumba zao.
Baada ya machafuko hayo kutulia na kuundwa serikali ya mseto kati ya vyama viwili hasimu, manusura na ndugu wa wahanga wa machafuko hayo walitaka kutekelezwa uadilifu kuhusiana wale wote waliohusika na mauaji ya baada ya uchaguzi. Mara ya kwanza ilikuwa tarehe 15 Disemba mwaka 2010 ambapo Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) ilimtambua Uhuru Kenyatta kuwa mmoja wa washukiwa katika jinai dhidi ya binadamu huko Kenya. Hata hivyo Uhuru Kenyatta kupitia kwa wakili wake, alipinga tuhuma hizo mbele ya Mahakama ya ICC huko Uholanzi na kusema Raila Odinga aliyekuwa Waziri Mkuu wakati huo ndiye alkiyehusika na machafuko na mauaji ya baada ya uchaguzi wa mwaka 2007. Katika uchaguzi huo Uhuru Kenyatta alimuunga mkono mpinzani wa Odinga Bwana Mwai Kibaki ambaye ni kutoka kabila la Kikuyu.
Mwaka 2012 wakati mahakama ya ICC ilipotangaza kuwa Uhuru Kenyatta ana kesi ya kujibu katika mahakama hiyo kulijitokeza wasiwasi mkubwa nchini Kenya na katika nchi nyingine za Afrika. Wakati huo wachambuzi wa mambo walitabiri kuwa faili hilo la Uhuru Kenyatta katika mahakama ya ICC lingepelekea kupungua kura zake katika uchaguzi wa Rais wa Machi mwaka 2013 na wapinzani walitaka mwanasiasa huyo asishiriki katika uchaguzi huo. Hata hivyo Uhuru alishiriki na kushinda uchaguzi na baadaye alitoa hotuba katika mkutano wa viongozi wa Afrika akiishambulia Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ambayo mwangwi wake ulisikika kote Afika na ulimwenguni kwa ujumla. Kenyatta alisema kuwa mahakama hiyo ni wenzo wa wakoloni na mabepari. Viongozi wa nchi za Afrika pia waliungana na Uhuru Kenyatta na kuzitaka nchi zote za bara hilo kujiondoa katika Hahakama ya Kimataifa ya Junai. Viongozi hao walisema mahakama hiyo inawafuatilia na kuwahukumu Waafrika tu na kufumbia jicho wahalifu wakubwa kutoka mabara mengine hususan Ulaya na Marekani.
Taarifa iliyotolewa na mahakama ya ICC imesema kuwa ukosefu wa ushahidi wa kutosha dhidi ya Uhuru Kenyatta ndiyo sababu na kufutiwa tuhuma.  Hata hivyo mahakama hiyo imesisitzia kuwa iwapo kutapatikana ushahidi mpya au kama mashahidi wa mauaji ya baada ya uchaguzi wa Kenya watakuwa tayari kutoa ushahidi mahakamani basi faili la kesi ya Uhuru Kenyatta litafunguliwa upya.
Share on Google Plus

About NELSON PASCHAL KAMUGISHA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

CREATED AND DESIGNED BY NELLYPAKA(WWW.NELLYPAKA.BLOGSPOT.COM)