
Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf ametangaza kwamba ugonjwa wa Ebola
umedhibitiwa lakini usaidizi zaidi wa jamii ya kimataifa unahitajika
kuhakikisha kuwa ugonjwa huo haurudi nchini humo baada ya kuangamizwa.

Ameiambia BBC kwamba kuimarisha mfumo wa afya ni muhimu.
Bi
Johnson Sirleaf amekiri kwamba alifanya makosa wakati wa kuzuka kwa
ugonjwa huo kama vile kupiga marufuku mikutano ya hadhara bila ya
kuwaelezea raia.
Kumekuwa na ongezeko la ripoti za maambukizi
mapya katika kipindi cha wiki mbili zilizopita katika mataifa yote
matatu yaliokuwa na ugonjwa wa Ebola ikiwemo,Liberia,Guinea na Sierra
Leone.
Zaidi ya watu 9000 wamefariki kutokana na ugonjwa huo tangu Disemba mwaka 2013.
About
NELSON PASCHAL KAMUGISHA
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment