
Rais wa Misri Abdul Fattah al-Sisi
ametoa ombi la kuwaondosha kwa ndege raia wa Misri wanaoshi nchini
Libya,baada ya wapiganaji wa Jihad kuchapisha picha katika mtandao
wakisema wamewateka raia 21 wa kanisa la Coptic.
Picha hizo
zinaonyesha watu hao wakiwa wamevalia nguo za rangi ya machungwa
wakitembezwa katika ufuo wa bahari na watekaji wao walioficha nyuso zao.Mtandao huo unaoshirikishwa na kundi la Islamic State umewaelezea watu hao kama wana kampeni wa kanisa hilo la Coptic na kusema kuwa kukamatwa kwao ni kulipiza kisasi kile wanachokitaja kuwa utekaji na unyanyasaji wa wanawake waislamu unaotekelezwa na kanisa la Coptic nchini Misri
Waziri wa ,maswala ya kigeni nchini Misri amewataka raia wa Msri kutosafri nchini Libya.
0 comments:
Post a Comment