Michuano ya ligi ya mabingwa barani
Ulaya, hatua ya kumi na sita bora, iliendelea Jumatano usiku kwa
kuzikutanisha timu za FC Basel ya Uswisi na FC Porto ya Ureno katika
mchezo ambao FC Basel ndio waliokuwa wenyeji na mchezo wa pili ukiwa
kati ya wenyeji Schalke 04 ya Ujerumani dhidi ya mabingwa watetezi Real
Madrid ya Hispania.
Tuanze na mchezo wa FC Basel dhidi ya FC
Porto. Mpambano huo ulimalizika kwa matokeo ya sare ya bao 1-1. Wenyeji
FC Basel ndio waliokuwa wa kwanza kujipatia goli katika dakika ya 11
likifungwa na Gonzalez ambalo lilidumu hadi kipindi cha pili, FC Porto
waliposawazisha katika dakika ya 75 kwa mkwaju wa penalti iliyofungwa na
Danilo baada ya mchezaji wa FC Basel Samuel Walter kuunawa.
Katika
mchezo huo ambao ulitawaliwa kwa kiasi kikubwa na wageni, FC Porto
wakimiliki kwa asilimia 63% huku wenyeji wakiwa na asilimia 37%
ulimalizika kwa mwamuzi wa mchezo huo Clattenburg kuwaonya wachezaji
tisa kwa kadi za njano, watano wakiwa ni wa FC Basel na wanne kutoka FC
Porto.
Kocha Carlo Ancelotti wa Real Madrid akishangilia goli na wachezaji wake
Mchezo mwingine ulikuwa katika
dimba la wenyeji Schalke 04 dhidi ya Real Madrid, ambapo Real Madrid
waliibuka kwa ushindi wa mabao 2-0 yakifungwa na Cristiano Ronaldo na
Marcelo. Real Madrid walipata goli lao la kuongoza dakika ya 26
likifungwa na Ronaldo na goli la pili lilifungwa na Marcelo dakika ya 79
ya mchezo.
Ronaldo amekuwa na magoli 58 katika michezo 58 ya ligi
ya mabingwa. Mpaka sasa Real Madrid inaongoza katika hatua hii ya kumi
na sita bora kwa michezo ambayo tayari imechezwa na timu nane tangu
itimue vumbi hapo juzi Jumanne usiku.
Real Madrid ilitawala mchezo
huo kwa asilimia 61% huku Schalke wakimiliki kwa asilimia 39%. Mwamuzi
wa mchezo huo Martin Atkinson aliweza kuwazawadia kadi za njano
wachezaji wanne, watatu kutoka Schalke na mmoja ni wa Real Madrid.
Michezo
inayokuja itachezwa tarehe 24 na 25 mwezi huu kwa Juventus ya Italia
kuialika Bor Dortmund ya Ujerumani na Man City ya England ikiwakaribisha
Barcelona ya Hispania. Na tarehe 25 itakuwa patashika nguo kuchanika
kwa Arsenal ya England kucheza na Monaco ya Ufaransa huku Bayer
Levkusern ikipepetana na Atletico Madrid ya Hispania.
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment