
Rais wa Ukraine Petro Poroshenko,
amevitaka vikosi vya umoja wa mataifa vya kulinda amani kupelekwa
mashariki mwa nchi hiyo ili kuhakikisha zoezi la kusitishwa kwa mapigano
linafanikiwa.
Ametoa wito huo katika mkutano maalum wa dharura wa
baraza la usalama, baada ya vikosi vya Ukraine kujitoa katika mji wa
mashariki wa Debaltseve kufuatia mashambulizi yaliyofanywa na waasi
wanaoungwa mkono na Urusi. Pande zote mbili zimekuwa zikilaumiana kwa
kukiuka makubaliano ya kusitishwa kwa mapigano yaliyofikiwa wiki
iliyopita.
Kwa upande wake, serikali ya Marekani imesema Urusi na
kundi la waasi linaloliunga mkono wameshindwa kutimiza makubaliano
yaliyosainiwa wiki iliyopita na viongozi wa Ujerumani, Ukraine, Ufaransa
na Urusi.
Viongozi hao wanne walipanga kujadiliana kuhusu mustakbali wa eneo hilo jana usiku.
Awali msemaji wa kansela wa Ujerumani Angela Merkel, amesema makubaliano hayo yanapitia wakati mgumu.
About
NELSON PASCHAL KAMUGISHA
This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
0 comments:
Post a Comment