TENGENEZA BLOG BOMBA SASA..

Rais wa Tunisia amtimua balozi wa Marekani

Rais Beji Caid Essebsi wa Tunisia amemtimua ndani ya Ikulu ya Rais, Jacob Walles Balozi wa Marekani nchini humo. T
aarifa zinasema kuwa, tukio la kutimuliwa Balozi wa Marekani ndani ya Ikulu ya Rais wa Tunisia limejiri  baada ya Balozi Walles kumweleza Rais Essebsi mpango wa Washington wa kutaka kujenga kambi ya kijeshi nchini Tunisia, ambao ulipingwa vikali na Rais Essebsi. Duru za habari zinasema kuwa, Rais Essebsi alikasirishwa sana na matamshi ya balozi wa Marekani mjini Tunis kiasi kwamba alikataa kuzungumza kwa njia ya simu na Rais Barack Obama wa Marekani baada ya kuombwa kufanya hivyo.
Essebsi mwenye umri wa miaka 88 alishinda kwenye duru ya pili ya uchaguzi wa rais uliofanyika mwaka jana nchini Tunisia, baada ya kujipatia asilimia 55.68 za kura zote. Rais Essebsi ambaye aliwahi kushika nyadhifa nyeti kama vile Waziri Mkuu, Waziri wa Mambo ya Ndani, Waziri wa Ulinzi na Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje katika utawala wa zamani wa Tunisia, alirejea tena kwenye ulingo wa kisiasa kupitia chama cha Nidaa Tounes.
Share on Google Plus

About NELSON PASCHAL KAMUGISHA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

CREATED AND DESIGNED BY NELLYPAKA(WWW.NELLYPAKA.BLOGSPOT.COM)