TENGENEZA BLOG BOMBA SASA..

Tanzania yaitahadharisha Burundi kuhusu machafuko

Marais Kikwete (kushoto)  na Nkurunziza Nchi mpatanishi wa amani Tanzania imetahadhsrisha kuhusu hatari ya kuibuka tena machafuko huko Burundi iwapo wanasiasa wa nchi hiyo hawataheshimu katiba ambayo itamzuia rais wa nchi hiyo kugombea kiti cha urais kwa mara ya tatu. Kwa mujibu wa katiba ya Burundi na makubaliano ya amani yaliyohitimisha vita vya ndani nchini Burundi vya zaidi ya muongo mmoja, ni kuwa hakuna mtu yoyote anayeruhusiwa kuwa rais kwa zaidi ya miaka kumi.
Hata hivyo wafuasi wa Rais Pierre Nkurunziza ambaye amekuwa madarakani Burundi tangu mwaka 2005, wanapinga suala hilo kwa hoja kuwa, muhula wa kwanza wa Nkurunziza haupasi kuhesabiwa kwa kuwa aliteuliwa na wabunge na si kwa kura za raia. Rais Jakaya Mrisho Kikwete wa Tanzania amesema kuwa, iwapo watu watakiuka katiba na mkataba wa amani wa Arusha, basi ipo hatari ya kuibuka upya machafuko huko Burundi ambayo yatakuwa vigumu kuyasitisha. Rais wa Tanzania aliyasema hayo jana usiku pambizoni mwa ziara yake ya siku mbili nchini Burundi.
Share on Google Plus

About NELSON PASCHAL KAMUGISHA

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments:

Post a Comment

CREATED AND DESIGNED BY NELLYPAKA(WWW.NELLYPAKA.BLOGSPOT.COM)