Ikiwa machungu ya Watanzania bado hayajapoa kutokana na kashfa ya
Sh306 bilioni kutoka katika Akaunti ya Tegeta Escrow, ufisadi mwingine
wa zaidi ya Sh252 bilioni umeibuliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa
Hesabu za Serikali (CAG), Profesa Mussa Assad ndani ya Wizara ya Ujenzi
ya Tanzania. Ukaguzi maalumu uliofanywa na ofisi ya (CAG) katika kipindi
cha mwaka wa fedha 2010/11 na 2011/12 umebaini kuwa taarifa iliyotolewa
na Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli, bungeni Novemba 2013 kuwa fedha
hizo zilitumika kwa miradi ya ujenzi wa barabara, haikuwa sahihi.Kutokana na ufisadi huo, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) amependekeza hatua stahiki zichukuliwe kwa wahusika wa Wizara ya Ujenzi na wakala wa barabara ili kuleta imani na uwazi kwa jamii na wahisani kuhusu bajeti.



0 comments:
Post a Comment